JINSI YA KUMFANYA MUMEO AWAHI KURUDI NYUMBANI


Inawezekana ukawa upo kwenye mahusiano yenye changamoto ya Mume wako kuchelewa kurudi nyumbani, Zifuatazo ni njia ambazo zinaweza kukusaidia kumrejesha mapema nyumbani.

Jambo la kwanza ni vizuri ukajiuliza kama kweli upo katika ndoa sahihi, kwa kutizama chanzo cha mahusiano yenu ni kitu gani kilichowaunganisha lakini Pia ukajiuliza bila kujidanganya wewe na Mumeo mnafahamu maana halisi ya mapenzi ?

Baada ya maswali hayo naomba ufahamu kwamba mapenzi yoyote yale lengo lake kubwa ni kuleta utulivu na kuhurumiana.

Je ndoa yako inakupa utulivu na mnahurumiana?, kama mnahurumiana iweje Mumeo achelewe kurudi nyumbani huku akijua fika kwamba wewe Mkewe hupendi achelewe kurudi nyumbani na kuchelewa kwake kunakuondolea utulivu ?.

Hatua Zifuatazo zitakusaidia kumrejesha Mumeo nyumbani mapema:

Je wewe sio chanzo cha Mumeo kuchelewa kurudi nyumbani? Na kama wewe unachangia kwa namna yeyote ile basi rekebisha yale asiyoyapenda Mumeo na hapo utakuwa umemaliza tatizo.Pambana na tatizo na sio Mtu, tambua tatizo, tafuta elimu ya tatizo husika ili upande daraja.Kuwa mvumilivu, mwenye hekima, busara, msikivu, mwenye kusamehe na kusahau.Kiri makosa yako na omba msamaha.Kubali kushindwa na usiwe mshindi kila siku hata kama umeshinda.Penda kabla hujapendwa.Toa kabla hujapokea.Japo inauma lakini usimuulize alikuwa wapi na kwa nini amechelewa kurudi.Mkaribishe kwa bashasha na mpe pole ya huko alikotoka.Hakikisha anakukuta ukiwa msafi na mwenye mvuto kama vile umerudi kutoka matembezi.Mpe chakula na kaa ule pamoja nae na kama ulishakula kaa karibu yake.Onesha kama vile unafurahia yeye kuchelewa kurudi, japo unaumia kwa ndani.Usioneshe kama vile una wivu wa yeye kuchelewa kurudi, bali onesha kuwa unahofia usalama wake anapochelewa kurudi.Usimnyime tendo la ndoa hata kama kachelewa kurudi na furahia tendo hilo kama vile ulikuwa ukimsubiria kwa hamu.Anapotoka onesha kama vile na wewe utatoka lakini usitoke bila ridhaa yake.





Comments