Wanawake wengi wanadhani kuwa wanaweza kumpangia mwanaume namna ya kulea mtoto wake ambaye alizaa nnje ya ndoa, namna ya kuwasiliana na Mama wa mtoto, namna ya kumhudumia Mama wa mtoto wake ila ukweli nikuwa hawawezi. Mtoto akishazaliwa anakua na haki zote sawa na mtoto wa ndani ya ndoa, ni mtoto wake na kiwango cha DNA ni kile kile.
Unapokubali kuwa mume wako, mpenzi wako au mchumba wako kazaa na mwanamke mwingine basi kubali pia kuwa, huyo mwanaume ataendelea kuwasiliana na huyo mwanamke aliyezaa naye mpaka wanaingia kaburini. Yaani mawasiliano yao yatakoma pale ambapo mmoja wapo kati ya watatu anakufa, awe ni mwanaume wako, mtoto au mwanamke.
Ubaya ni kwamba, huwezi kumpangia mwanaume eti asiongee na Mama wa mtoto wake, eti asiende kumuona mtoto, eti asimpost mtoto, asimsomeshe na vingine vingi. Ukipata mwanaume anayejielewa basi jua atajiheshimu, atawasiliana na huyo mwanamke mwingine kimya kimya na hatakuambia chochote. Ukipata ambaye hajielewi basi jua kuwa atakua anaongea naye mbele yako, anampost mwanamke kila siku na vitu vingine vingi. Najua inauma ila ndiyo ukweli, kuna wale wanasema basi ili asiwasiliane na Mama wa mtoto basi umchukue mtoto umlee wewe!
Hawa ndiyo wanachekesha, hivi hata ukimchukua mtoto unadhani huyo mwanamke ni mjinga kiasi gani, anaweza kulala mwezi mzima bila kujua mtoto wake anaendeleaje, hivi kweli wewe ni mwanamke, ukimuacha mtoto wako kwa Mama yako mzazi ambaye unamuamini lakini utanpiga simu kutwa mara tatu kama dozi ya UTI sembuse umempeleka mtoto wako umpeleke kwa Mama wa kambo ambaye mnanuniana!
Kuna mtu juzi alisema ukinisoma si lazima kukubaliana na ushauri wangu, akili ya kuambiwa changanya na yakwako. Ni kweli, hata na wewe wakati unasomaComment acha kuhcukua kila kitu, akili ya kuambiwa changanya na yako, kuna wanawake wengi huko kwenye comment wanasema kuwa naachana naye ila wakinipigia simu wanavumilia, sisemi uvumilie ila changanya na yakwako!
Najua ni Ngumu ila ndiyo ukweli, achene kuwa mashamba darasa, kama unasamehe samehe kama unaondoka ondokaa cha kuwa katikati!
Comments
Post a Comment