Katika dhana isemayo makubaliano ni muhimu kwenye tendo la"ndoa"
Nimegundua kwamba mwanamke huwa kama pasi huchelewa kupata joto na hutunza joto kwa muda zaidi hata baada ya kumaliza kupiga pasi.
Mwanaume ni rahisi kusisimka kimapenzi wakati mwanamke huhitaji kusisimuliwa.
Mwanaume husisimuliwa na moja ya mlango wake wa fahamu kupitia kuona wakati nwanamke husisimuliwa kupitia milango yote mitano ya fahamu Kuguswa, kusikia, kuona, kuonja, kunusa na wororo wa mwanaume.
Mwanaume ni mfano wa bulb ya umeme uki-switch tu mara moja inawaka wakati mwanamke ni mfano wa pasi ya umeme ambayo huchukua muda hadi ipate joto na hutumia muda zaidi to cool off.
Hii ni muhimu sana ukitaka kuwa mpenzi mzuri na mpenzi mzuri hujua na kuzingatia jinsi ya kumridhisha mwenzake.
Mwanamke anaongozwa na highway ya emotions, atajisikia vizuri sana kama alikuwa na idea kwamba kutakuwa na kuwasha pasi yake ya umeme mapema.
Itakuwaje kama wakati wa kuondoka asubuhi mume akampa mke busu la uhakika na kumnong'oneza mkewe kwamba vipi unaonaje leo usiku ukawasha pasi mapema kwani nina hamu sana kupiga pasi nguo kwani naona bulbu yangu ina mwanga wa uhakika leo".
Nahisi mke atashinda cku nzima akijiandaa jinsi ya kuhakikisha pasi yake inawaka chapchap usiku na ikitokea na mchana akaambiwa neno lingine mwororo inaweza kuwa jioni yenye mwako wa mahaba.
Kwa mawasiliano mazuri na kupeana quality time mwanamke huweza kufunguka kiakili, kimwili na kiroho na kuwa tayari kwa usiku wa kufurahisha na kuridhishana.
Ndiyo maana wakati mwingine ukipapasa usiku unaambiwa ?baba nanii leo kichwa kinaniuma sana? au ?nimechoka sana? au ? na kuambiwa maliza haraka? au pasi inakuwa kavu kabisa matokeo yake ni pasi inagoma kuwaka na kuanza kuumizana.
Jifunze kuwa mwanaume mwororo wasiliana na mke, tafuta muda wa kumsikiliza, cheka naye, cheza naye, ongea naye, mguse na mkumbatie na kumbusu hata kama si wakati wa sex ni wako na ni wewe uliamua kuishi naye.
Comments
Post a Comment