Zijue aina tano za mahusiano ya kimapenzi

 


Wanasaikolojia mbalimbali wamejaribu kuelezea aina za mahusiano ya kimapenz ambayo wapenzi wawili wanaweza kuwa wanayapitia katika kipindi flani cha mahusiano yao. Lakini kabla hatujaangalia hizi aina lazima tujue kuna vitu vitatu vinavounda na kudetermine ni aina gani ya mahusiano ya kimapenz watu wako nayo kwa mda huo.

Kuna kitu kinaitwa TRIANGULAR THEORY OF LOVE yaani Intimacy,Commitment na mwisho kabisa ni Passion. Ntajaribu kuelezea kwa ufupi kila kimoja kabla sijaingia kwenye point ya msingi yenyewe.

Intimacy. Hii ni hali ya kuwa karibu kihisia na mpenz wako,Kuna hali flani hivi hutokea yaani unakuta mnashare the same feelings.Sijui ka ishakutokea unataka tu kumpigia simu mpenz wako ghafla unakuta naye anakupigia,nafsi zenu zinakuwa zinaongea na unajikuta unachowaza wewe ni sawa cha mwenzi wako.

Commitment. Hali ya mtu kuhakikisha uhusiano na mpenzi wake unabaki salama hata iweje.Mtu hapa anaweza kuwa katika uhusiano lakini asiwe committed kwa lolote kuhakikisha uhusiano unadumu kwa mda mrefu.Yupo na anakupenda lakini ikatokea chochote mkaachana ye sawa tu.

Mwisho kabisa ni Passion.Kitu kinachoweza kukusukuma uwe katika hali ya kimahaba na mpenzi wako. Muonekano wako kimwili inaweza kuwa macho mazuri kwa mwanamke,wengine makalio nk au unakuta kifua kizuri au muonekano maridadi kwa mwanamme.

BAADA YA KUANGALIA TRIANGULAR THEORY OF LOVE,Tuangalie sasa aina mahusiano ya kimapenzi na hizi aina zinategemea kwa kiasi kikubwa hizo three components. Yaani intimacy,commitment na passion.

1. CONSUMATE LOVE: Hi ni aina ya mahusiano ya kimapenzi ambapo kuna zote hizo components tatu yaani intimacy,commitment na passion. Na kujua kama mko katika aina hii ni pale mnapoweza au kufurahia sex or any physical affection,kila mtu yuko committed kuhakikisha mnafika mbali mna mda mzuri wa kuwasiliana,kila mtu anaweza kushow ni kitu gan kinamvutia toka kwa mpenzi wake na kuonesha positive response. Kiujumla hii ndo daraja la juu kabisa katika aina za mahusiano ya kimapenzi.

2. COMPANIONATE LOVE: Hii inahusisha two components yaani Intimacy na Commitment.Utaona hapa Passion hamna na aina hii hutokea sana kwa wale marafiki wa karibu mno na mwisho hujikuta wanakuwa na Malengo yao ya mbali na inaweza kuwa kuoana. Mtu yuko ktk mahusiano unamuuliza umempendea nn huyo unakuta hana cha kukueleza zaid atakuambia nampenda tu.Hapa mtu aangalii physical attractions zozote zile lakini yuko committed kuhakikisha wanaishi pamoja mda wote na anampenda sana. Utakuta mwanamke anasura mbaya au mwanaume yupoyupo tu ila kutokana na kuwa karibu kwa muda mrefu wanajikuta wako katika mahusiano.

3. EMPTY LOVE: Hakuna Intimacy na Passion. Hapa kuna commitment tu.Unaishi na mtu huna hisia naye hata kidogo wala hata sexual attractions zozote kwake huzioni zaidi unachowaza ni kuishi nae tu.Hakuna kujuliana hali na inaweza pita hata siku au wiki hata huoti chochote wala kumwaza mpenzi wako. Na hii hutokea sana kwa wanandoa,unakuta baba anachojua ni kuacha hela ya mboga mezan tu na akirudi hata wazo na wewe hana na hata upande wa mwanamke anachojua ni kumpikia mmewe kama wajibu wake na kuweka mezani kisha kuendelea na shughuli zake.No intimacy no passion.

4.ROMANTIC LOVE: Katika hii aina tunaona kuna Intimacy na Passion tu,hakuna commitment. Hapa kuna kushare vitu vingi sana na mahaba yenye hisia kali sana sema huwa hayana mipango mirefu au hayadumu sana coz no commitment. Na haya huwa hayafiki mbali sana.

5. INFATUATION: Hapa kuna Passion tu,no intimacy wala commitment. Infatuation ni Ile hali ya kuvutiwa na mtu flani kimapenzi kutokana hasa na physical attractions,mfano unaweza mwona mwanamke may be anashape kali tayari ukawa umevutiwa naye hiyo tunasema infatuation na haiwez kuwa LOVE coz kuna possibility kile kitu ulichovutiwa nacho kikapotea na hutamtaka tena. Na hii huwa haidumu sana sababu physical attractions may change according to the environment.Umemwona mwanamke au mwanaume anapendeza we ukamlukia mwisho akifulia lazima umkimbie tu coz kilichowaunganisha pale ni physical attractions na sio vingine yaani no intimacy no commitment.





Comments